Aliyekua nahodha na mshambuliaji wa klabu ya Simba, Mussa Hassan Mgosi amesema kikosi cha klabu hiyo hakikustahili kushinda bao moja kwa sifuri katika mchezo wa jana dhidi ya Young Africans, na badala yake kilipaswa kuibuka na ushindi wa zaidi ya mabao matano kwa sifuri.

Mgosi ambaye alikua shuhuda wa mchezo huo uliounguruma Uwanja wa Taifa, Dar es salaam, amesema kutokana na kiwango cha kikosi cha Simba na uwezo wa mchezaji mmoja mmoja, ushindi wa bao moja ni kiduchu na wala hakuridhika nao.

Hata hivyo Mgosi ambaye pia aliwahi kuzitumikia klabu za JKT Ruvu (JKT Tanzania) na Mtibwa Sugar, amesema pamoja na kutoridhisha na idadi ya mabao, kwa upande mwingine amefurahia upatikanaji wa point tatu mhimu za mchezo huo, ambao ulikua unasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka ukanda wa Afrika mashariki na kati.

“Simba ilistahili kupata ushindi wa mabao 6-0 lakini walishindwa kutumia vizuri nafasi walizotengeneza.

“Yanga walicheza kwa kujilinda sana muda mwingi walikuwa nyuma, kama Simba wangetumia mapungufu hayo wangepata ushindi mkubwa wa kihistoria jana.”

“Nimefurahi kuona Simba inapata pointi tatu muhimu lakini sijaridhika na ushindi kiduchu waliopata, wangefunga mabao mengi zaidi” Amesema Mgosi.

Ashikiliwa na polisi kwa tuhuma za mauaji
Hans Poppe, Mkandarasi wa uwanja wa Bunju kufikishwa Mahakamani

Comments

comments