Rais wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Ally Mohamed Shein amewaasa Wanzanzibar kutokufanya makosa wakati wa uchaguzi wa Oktoba 28, mwaka huu kwa kuchagua kiongozi mwenye maslahi binafsi na badala yake ni vyema wakamchagua Mgombea mwenye uwezo.

Shein ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi za CCM zilizofanyika uwanja wa Demokrasia kibanda maiti, akimnadi mgombea urais Zanzibar kupitia chama cha mapinduzi (CCM). Dkt. Hussein Ally Mwinyi kuwa ataitekeleza ilani ya chama hicho bila kusita.

“Mzingatie haya, msije mkafanya makosa ya kujaribu uongozi kumpa mtu ambae hana uwezo. kumpa mtu ambae anatamaa yake binafsi,” amesema Shein.

Aidha, Shein amesema kuwa Mwinyi ataendeleza mapinduzi ya Zanzibar na kuwataka wazanzibar kumchagua mtu kwa kujua uwezo wake.

CCM leo Septemba 12, imezindua rasmi kampeni zake za uchaguzi mkuu Zanzibar, utakaofanyika Oktoba huku ikiwa na wagombea 17 wanaowania kuchaguliwa katika nafasi ya urais.

.

Stevie Lee: Nyota na mpambanaji wa Jackass afariki
50 wahofiwa kufariki kwa kuangukiwa na mgodi wa dhahabu DRC