Mwanafunzi wa kidato cha nne katika Kaunti ya Bomet nchini Kenya ameuawa kwa kuchomwa na kisu shingoni baada ya kutokea ugomvi kati yake na mwanaume mmoja kuhusu mwanamke.

Mkuu wa eneo la Siongiroi, Joseph Ngeno amethibitisha kutokea kwa tukio hilo akieleza kuwa wasamaria wema walimkimbiza kijana huyo katika kituo cha afya cha Siongiroi kujaribu kuokoa maisha yake, lakini alipoteza maisha.

“Jeraha lilikuwa kubwa sana, ambapo inaonesha alichomwa na kisu chenye ncha kali mara mbili shingoni, damu nyingi ilitoka na kusambaa eneo lote alilokuwepo, na matone yalidondoka hadi katika kituo cha afya cha Siongiroi,” Ngeno alieleza.

Alieleza kuwa mwanamke aliyesababisha kutokea kwa ugomvi huo hakuwa mwenyeji wa eneo hilo, anadaiwa kutoweka ghafla baada ya wanaume hao kuumizana.

Marehemu ametajwa kama mwanafunzi wa kidato cha nne wa Shule ya Sekondari ya Kapsinendet iliyoko Chepalungu.

Jeshi la Polisi la eneo la Chebunyo limewaambia waandishi wa habari kuwa wanamshikilia mtu mmoja kutokana na tukio hilo akisaidia upelelezi.

Mtendaji Serikali ya Mtaa Mbezi Msumi Achinjwa ofisini kwake
Ukatili wa kijinsia mtandaoni wawatesa wasichana