Mjumbe wa Bodi ya wakurugenzi wa kampuni ya uchimbaji ya Acacia, Balozi Juma Mwapachu amestaafu nafasi hiyo baada ya kuitumikia kwa vipindi viwili.

Mwapachu amechukua uamuzi huo leo, julai 13 baada ya muhula wake wa pili wa miaka mitatu wa ujumbe wa bodi hiyo kumalizika.

Taarifa iliyotumwa leo na bodi ya Wakurugenzi na Menejimenti ya Acacia imeeleza kuwa inamshukuru Balozi Mwapachu kwa utendaji wake na ushirikiano wake wote alioutoa kwa hali na mali pindi alipokuwa mjumbe.

”Tunamtakia maisha mema,” imesema taarifa hiyo.

Kutokana na mabadiliko hayo, Bodi ya Acacia itabaki na wajumbe saba, wakiwemo wanne wakurugenzi na watatu wasio wakurugenzi

TRA yaifungia Radio Free Africa (RFA)
Masamaki na wenzake 5 waachiwa huru sakata la TRA