Mwandishi habari maarufu nchini Cameroon, Martinez Zogo ambaye alitoweka katika mazingira ya kutataniasha kukufuatia kile ambacho Umoja wa haki za vyombo vya habari lilikiita utekaji, amepatikana akiwa amekufa.

Zogo, ambaye alikuwa Meneja wa kituo Binafsi cha Redio cha jijini Yaounde, Amplitude FM na mtangazaji nyota wa kipindi maarufu cha kila siku cha Gridlock amekutwa amefariki huku chanzo cha kifo chake kikiwa bado hakijafahamika.

Mwandishi habari maarufu nchini Cameroon, Martinez Zogo. Picha ya Actu Cameroon.

Mwanahabari huyo aliyekuwa na umri wa miaka 51, kabla ya kutoweka kwake alifanya kipindi kilichozungumzia ufisadi, na bila kusita aliuliza maswali kwa kuwataja watu mashuhuri na kisha alitoweka tangu Jumanne wiki iliyopita (Januari 17, 2023).

Shirika la Waandishi Wasio na Mipaka nchini Cameroon (RSF), limesema gari la Zogo lililokuwa limeharibika vibaya, lilipatikana nje ya kituo cha Polisi katika viunga vya mji mkuu, Yaounde siku ya Jumanne.

Hakuna atakayefungwa kwa kukosa Bima ya afya: Ummy
Abdallah Bares anukia Tanzania Prisons