Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega ameitaka Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Handeni Mkoani Tanga, kukomesha mara moja wizi wa mifugo unaofanywa wilayani humo ikiwemo katika Ranchi ya Mzeri ili wafugaji waweze kunufaika na uwekezaji wao.

Ameyasema hayo wakati wa ziara ya kikazi ya siku moja katika ranchi hiyo iliyo chini ya Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) huku akisistiza kusikitishwa kitendo cha wizi wa mifugo kilicholalamikiwa na baadhi ya wawekezaji waliopatiwa vitalu katika ranchi hiyo.

Aidha Naibu Ulega amemtaka Kamanda wa Polisi Wilaya ya Handeni kuhakikisha anakomesha vitendo hivyo vya wizi na endapo mtu akibainika na makosa ya uwizi sheria ichukue mkondo wake.

“Nimefarijika sana OCD aliponiambia nataka nikuambie Naibu Waziri hapa mimi nipo katika kusimamia haki vituo vyote ambavyo kesi na malalamiko yamekuwa mengi amesema atasimamia vyema malalamiko yote yakiwemo ya watu wanaofanya vitendo hivyo kuendelea kufanya licha ya kuchukuliwa hatua za kisheria,” Amesema Naibu Ulega

  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (Mb), (kulia) akiangalia pembe la ng’ombe anayedaiwa kuibwa na kuchinjwa kutoka katika Ranchi ya Mzeri siku moja kabla ya kuanza ziara yake ya kikazi Wilaya ya Handeni Mkoani Tanga na kuutaka uongozi wa wilaya hiyo kukomesha mara moja vitendo vya wizi wa mifugo.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (Mb), (kushoto) akimpa maelekezo Meneja wa Ranchi ya Mzeri Mberwa Lutagwelera wakati alipofanya ziara ya kikazi ya siku moja katika ranchi hiyo iliyopo Wilaya ya Handeni Mkoani Tanga.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega (Mb), akikagua ng’ombe waliopo katika Ranchi ya Mzeri iliyopo Wilaya ya Handeni Mkoani Tanga wakati alipofanya ziara ya kikazi ya siku moja katika ranchi hiyo iliyopo Wilaya ya Handeni Mkoani Tanga.

Serikali yatoa ufafanuzi Daktari aliyeanguka
Rais Samia azungumza na Eng Ahmed El Sewedy mwekezaji kutoka Misri