Azam FC imewalazimu kusubiri hadi dakika ya 89 ili kutimila mpango wa kuibuka na alama tatu za mchezo wa mzunguuko wa tatu wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi Namungo FC.

Azam FC ilikua nyumbani jijini Dar es salaam katika Uwanja wa Azam Complex Chamazi na ilitarajiwa kupata upinzani mkali kutoka kwa wageni wao Namungo FC.

Mshambuliaji kutoka DR Congo Idris Mbombo ndio amebakisha furaha nyumbani Azam Complex Chamazi likiwa bao lake la kwanza la Ligi Kuu tangu aliposajiliwa klabuni hapo miezi mitatu iliyopita.

Ushindi huo unaiwezesha Azam FC kufikisha alama 4, baada ya kushuka dimbani mara tatu mpaka sasa.

Namungo FC wamepoteza mchezo wa kwanza msimu huu, baada ya kuanza vizuri kwa kuifunga Geita Gold bao 1-0, kisha wakaambulia sare ya 1-1 dhidi ya Kagera Sugar na leo wameangukia pua kwa kufungwa bao 1-0.

Upande wa Azam FC walianza kwa sare ya 1-1 dhidi ya Coastal Union, kisha wakapoteza dhidi ya Polisi Tanzania kwa mabao 2-1.

Ni kweli Shatta Wale amefariki Dunia?
Mwamnyeto: Tulihimizwa kufanya kitu dakika 15 za mwanzo