Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Nape Nnauye  ameahidi kurudisha heshima ya michezo na pia kuhakikisha ubora wa viwanja unakuwa wa hali ya juu, akianzia na Uwanja wa Nyamagana wa jiji la Mwanza.

Aliahidi hilo wakati waziara yake juzi Mkoani Mwanza alipokuwa anauzungumzia uwanja wa michezo wa kihistoria wa Nyamagana. Alielezea kushangazwa na kudumaa kwa maendeleo ya uwanja huo, ikiwa ni pamoja na kusuasua kwa mradi wa kuwekwa kwa nyasi bandia.

“Nimeanza kushughulikia suala la nyasi za Nyamagana tangu nilipoingia madarakani, shida ninayoina hapa ni kwamba ukarabati mwingine unashindwa kuendelea kutokana na kutokuwepo kwa nyasi bandia.

“Sasa nyasi bandia nitalimaliza, mimi nashughulika nalo hilo lipo kwangu lakini haya maeneo mengine mpango ukoje?” Alihoji akimuuliza Ofisa Michezo wa Jiji la Mwanza, Mohammed Bitegeko.

Aliendelea kusema: “Hapa pana uzembe mkubwa ambao unaendelea, kila mtu ukimuuliza maendeleo ya huu uwanja anazungumza mambo ya nyasi bandia, lakini huu uwanja inaonyesha una awamu zaidi ya moja za ukarabati.

Hivi kila kitu kimesimamishwa na nyasi bandia? “Kwenye suala la nyasi bandia nawapongeza Jiji kwa kutoa fedha zenu. Mchakato ulivurugika juu kwa wakubwa huko kwa sababu TFF (Shirikisho la Soka Nchini) walipaswa kusimamia hili mapema,” alisema.

Aliongeza kuwa, TFF walipaswa kuzungumza na serikali mapema kwani kwa kawaida vifaa vya michezo haviingizwi bure, bali hulipiwa. Nape amemuomba Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella kushirikiana na Jiji la Mwanza katika ukarabati wa uwanja huo .

Aidha, Bitegeko alisema Halmashauri ya Jiji imeanza mazungumzo na TFF kuweza kupata michoro ya majukwaa na maeneo mengine ya ndani ya uwanja.

Video: TAKUKURU Waingiza Miguu Yote Sakata La upangaji Matokeo
Romelu Menama Lukaku Kuuzwa Kwa Masharti