Baada ya kufungiwa wimbo wake wa ‘Pale kati patamu’ Ney wa Mitego amesema kuwa ananyimwa uhuru wa kiuandishi hivyo anawaachia wanasheria wake waweze kumsaidia.

Akifanya mahojiano na Planet Bongo ya East Afrika radio Nay amesema huu ni wimbo wake wa tatu kufungiwa na BASATA hivyo kwa upande wake ameona ni tatizo la kisheria na ni kutokana na watanzania kutojua sheria.

”tunapoelekea kuna tatizo,naona pia haya  ni maamuzi binafsi ya kufungia nyimbo zangu, huu ni wimbo wangu wa tatu unafungiwa lakini wanasheria wangu na mimi pia tutalijadiliana na Basata ili nipate haki zangu”.-Nay.

Katibu Mkuu mtendaji Baraza la sanaa Taifa Geofrey Ngereza amesema Nay ameitwa kuchukua barua ya kumuita ili kuhudhuria kikao kitachojadili wimbo wake kukosa maadili yaliyosababisha kufungiwa .

godfrey-Mngereza

Aidha amesema katika mazungumzo hayo wataangalia utetezi wake pia adhabu zitatokana na utaratibu wa sheria za makosa ya aina hiyo hivyo watu wasubiri baada ya kikao watakachofanya ndipo watatangaza ni adhabu gani watatoa ikiwa ni pamoja hiyo iliyofanyika ya kufungia wimbo.

Kwa upande wake Nay amesemwa anashangazwa na Basata kufungia wimbo wake ambao vituo vya radio hawakuona kama una tatizo kuchezwa kwani uandishi aliotumia ni wa kutumia tafsida kama wengine.

Asilimia 60 nanyimwa uhuru wangu wa utunzi wangu, nanyimwa haki za uandishi nilichokiimba kwenye hapa kati patamu hakuna tofauti na aliyesema hainaga ushemeji, au yamoto walivyosema una rambo lakini kwangu imekuwa tatizo” alisema Nay.

 

 

 

Mke wa Trump azua jambo baada ya ‘ku-copy’ hotuba ya mke wa Obama
Shomari Kapombe Aanza Kujifua Taratibu