Nay wa Mitego amezungumzia wimbo wa Young Killer Msodoki wenye dakika mbili ‘True Boya’, uliotokana na jinsi alivyomchana rapa huyo kutoka Mwanza kwenye wimbo wake mpya ‘Fire’.

Nay alikiri kusikia shairi moja la Msodoki ambalo alidai ni jingo na sio wimbo, huku akisisitiza kuwa alichokisema kwenye wimbo wake wa ‘Fire’ ni ukweli mtupu na sio kuchamba. Alisema kuwa Young Killer ameshuka kimuziki  ingawa uwezo wake wa kuandika na kuchana bado ni mkubwa.

“Kama kusema ukweli ni kuchamba, basi wachambaji ni wengi,” alisema Nay wa Mitego.

“Nilichokiongea, wadau wa muziki wanalijua hilo, nina imani hata yeye analitambua hilo. Ndio maana unaona kila siku anapambana, anatoa wimbo huu na ule, mara awe Young Killer wa Mitego, naye anachana watu basi naye amekuwa mchambaji,” aliongeza.

Nay alisisitiza kuwa alichokiimba na aliowakwaruza kwenye wimbo wake wa ‘Fire’ ni ukweli mtupu, akitoa mfano kuwa Baraka Da Prince biashara yake ya muziki imeendelea kuporomoka.

Alisema kuwa wasanii hao wanapaswa kujiuliza walipokosea huku sehemu kubwa ya madai yake akidai ni kukosa nidhamu kwa waliowapandisha kwenye muziki.

Kabla ya kuachia ‘True Boya’, Young Killer alisema kuwa amekipokea alichokisema Nay wa Mitego kwenye wimbo wake wa ‘Fire’ na amekubali kuwa amemrekebisha, lakini naye asubiri atampa zawadi ya Eid kwa lengo la kumrekebisha pia.

Wabakaji kukomeshwa, adhabu kali yaja
El Hadji Diouf: Mimi sio mtu mbaya, Ulaya walinionea