Timu ya Taifa ya Vijana U-20 (Ngorongoro Heroes) wamepewa mapumziko ya siku tatu ili waweze kupumzisha miili yao ili waweze kujiweka sawa katika michezo inayokuja mbele yao.

Hayo yamewekwa bayana na Shirikisho la Mpira wa Miguu wa Tanzania (TFF) leo Aprili 24, 2018 baada ya wachezaji hao kuwasili nchini wakiwa wametokea nchini DR Congo kwenye mchezo  wake wa marudiano wa kufuzu fainali za Afrika za vijana U-20 dhidi ya DR Congo.

Hata hivyo, Ngorongoro Heroes katika raundi ya pili watacheza dhidi ya Mali mwezi ujao ambapo mchezo wao wa kwanza wakianzia katika dimba la nyumbani.

Uwanja wa Taifa kufunguliwa saa mbili asubuhi
Kocha Mwinyi Zahera atua Tanzania, azungumza na Young Africans