Nicki Minaj anadaiwa kufunga pingu za maisha kwa siri na mpenzi wake mpya, Kenneth Petty ambaye amekuwa naye kwa kipindi cha wiki kadhaa.

Kwa mujibu wa MTO News, ambayo Nicki ana uhusiano nayo imeeleza kuwa wawili hao walifunga ndoa lakini watu wasitegemee kuwa wataweka wazi mwaka huu.

“Nicki amefunga ndoa na Kenneth. Usiwatarajie kuweka wazi hivi sasa kwa sababu Nicki anajipanga kuanza ziara yake ya muziki. Tattoo aliyoichora kwenye mwili wake ilikuwa ni ishara ya tukio zito lijalo,” chanzo kimoja kimekaririwa na MTO.

Chanzo hicho kimeenda mbali na kueleza kuwa Nicki Minaj amebadili jina lake halisi na kuweka jina la mumewe huyo, yaani badala ya Onika Tanya Maraj sasa ni Onika Petty.

Tetesi hizo pia ziliwekwa kwenye mtandao wa Twitter na watumiaji kadhaa ambao ni wafuatiliaji wa masuala ya burudani ambao walidai pia kuwa mwaka kesho, yaani kuanzia wiki ijayo taarifa rasmi itatolewa.

Petty alikuwa wa kwanza kufanya tukio la aina yake kwa kujichora mwilini jina halisi la rapa huyo wa Barbie Tingz ambalo ni Onika.

Nicki ambaye alikuwa mpenzi wa Meek Mill na baadaye Nas kabla ya Petty, amewahi kusimulia kuwa amesumbuliwa na mapenzi ikiwa ni pamoja na kupigwa na manyanyaso mengine.

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Desemba 25, 2018
Aliyemwagiwa tindikali na mpenzi wake awaburuza polisi Mahakamani

Comments

comments