Mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda Emmanuel Okwi ameweka historia kubwa uwanja wa taifa mara baada ya kufunga jumla ya magoli manne kati ya magoli saba ya Simba dhidi ya klabu ya Ruvu Shooting katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kikosi cha Simba ambacho kinachonolewa na Kocha wake, Joseph Omog kilianza kwa mashambulizi makali ndani ya dakika za mwanzo za mchezo dhidi yaRuvu Shooting na kupelekea Emmanuel Okwi kuweza kupata bao la kwanza ndani ya dakika 18 huku dakika ya 22 akiongeza jingine.

Simba ilijipatia goli jingine tena dakika 35 kupitia kwa raia huyo wa Uganda hali ambayo iliifanya timu Ruvu Shooting kuchanganyikiwa na kucheza kwa kutoelewana uwanjani huku wakikosa mbinu za kufanya mashambulizi.

Aidha, Simba ilizidi kufanya mashambulizi makali dhidi ya Ruvu Shooting na katika dakika ya 42 Shiza Kichuya aliwainua tena mashabiki wa Simba kwa kupachika goli la nne huku Juma Liuzio naye aliweza kuipatia Simba goli la tano katika dakika ya 45 ya mchezo.

Vile vile kipindi cha pili kilipoanza Simba waliendeleza mashambulizi wakiwa na lengo la kutafuta zaidi magoli katika dakika ya 53 Okwi aliweza kuwapa furaha mashabiki wa Simba kwa kupachika goli la sita katika mchezo huku kwake yeye akiwa anatimiza goli la nne.

Wachezaji wa Simba hawakuridhika na magoli hayo waliendeleza mashambulizi na ndani ya dakika 80 ya mchezo Erasto Nyoni aliweza kuipatia Simba goli la saba, mpaka mpira unakwisha Simba walitoka kifua mbele kwa bao 7- dhidi ya Ruvu Shooting.

Video: Mahakama imetenda haki- Sakaya
Mayanga Ataja Taifa Stars Itakayoivaa Botswana