Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Mhandisi Kundo Mathew
akikagua na kutoa maelezo kuhusu Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano kwa Mbunge wa
Mtwara Mjini Mhe. Hassan Mtenga alipozuru katika bandari ya Mtwara tarehe 11.7.2021 ikiwa ni siku ya kwanza ya ziara yake ya siku tatu katika Mkoa huo ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano, ujenzi, uwezo na ubora wa minara ya mawasiliano, mwingiliano wa mawasiliano mipakani na usikivu wa redio ya Taifa TBC.
Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Mhandisi Kundo Mathew (wa tatu kulia) alipotembelea bandari ya Mtwara kwa lengo la kukagua miundombinu ya Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano uliofikishwa katika bandari hiyo kwa lengo la kuwezesha mawasiliano ya simu na intaneti yenye kasi kubwa na uwezo mkubwa Kulia ni Mbunge wa Mtwara Mjini Mhe. Hassan Mtenga akifuatiwa na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Dunstan Kyobya. Wengine ni wafanyakazi wa bandari na baadhi wataalam aliombatana nao
katika ziara hiyo
Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Mhandisi Kundo Mathew (wa pili kushoto) akimsikiliza Kaimu Meneja wa Bandari ya Mtwara Nobert Kalimbu (kushoto) wengine kutoka kulia ni Mbunge wa Mtwara Mjini Mhe. Hassan Mtenga akifuatiwa na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Dunstan Kyobya wakati wa kukagua ufikishaji wa miundombinu ya Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano bandarini hapo
Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Mhandisi Kundo Mathew
akizungumza katika kikao cha ndani katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mtwara kabla ya kuanza ziara yake wilayani humo ambapo alitembelea bandari ya Mtwara kukagua upatikanaji wa huduma za mawasiliano ya simu na Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano uliofikishwa bandarini hapo pamoja na kutembelea baadhi ya maeneo yenye changamoto ya mawasiliano ya simu katika kata ya Mitengo
Mbunge wa Mtwara Mjini Mhe. Hassan Mtenga akizungumza katika kikao cha ndani katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mtwara wakati Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Mhandisi Kundo Mathew alipotembelea Wilaya hiyo ikiwa ni siku ya kwanza ya ziara yake ya siku tatu katika Mkoa wa Mtwara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano, ujenzi, uwezo na ubora wa minara ya mawasiliano, mwingiliano wa mawasiliano mipakani na usikivu wa redio ya Taifa TBC.

Gomes atuma salamu kwa waliobaki
Serikali yakagua mkongo wa taifa bandari ya Mtwara