Jeshi la Polisi mkoani Kagera limewaua watu watatu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi katika kijiji cha Nyamaragara Kata ya Rusahunga wilayani Bihalamuro katika majibizano ya risasi kati ya Jeshi la polisi na majambazi hao.

Hayo yamesemwa na Kamanda wa polisi mkaoni humo, Revocatus Malimi ambapo amesema kuwa tukio hilo lilitokea tarehe 16 Machi baada ya mtu mmoja ambaye ametafutwa na jeshi la polisi kwa muda mrefu bila mafanikio baada ya kufanya uhalifu mwaka jana.

Amesema kuwa jambazi huyo aliyejulikana kwa jina la Shabani Manyotema [40] ambaye alikimbilia kijiji cha  Midao na baadaye akakamatwa ambapo aliliambia jeshi hilo kuwa kuna mtu anashirikiana naye kufanya uharifu ambaye ni raia wa Burundi aliyejulikana kwa jina la Erick Samsoni 19 anayeishi Benaco Ngara.

“Ilikuwa saa tatu usiku wakati watuhumiwa wakiendelea kutupeleka wanakoficha silaha, ndipo askari wetu alianza kushambuliwa na badaye watuhumiwa walianza kutoroka baada ya kukabiliana nao kwa majibizano ya risasi ndipo mtu mwingine akajeruhiwa katika eneo la tukio ambaye hajajulikana mpaka leo.”Amesema Malimi.

Aidha, ameongeza kuwa baada ya kukabiliana na wahalifu majeruhi wote 3 walipelekwa katika Hospitali ya wilaya ya Bihalamuro na badaye walifariki dunia wakiwa katika hospital hiyo.

Katika eneo la tukio Bunduki ya kivita aina ya AK47 yenye risasi 17 iliyokuwa ikitumiwa na wahalifu ilikamatwa pamoja na bunduki nyingine ya Magazine yenye risasi 8 pia ilikamatwa huku maganda 5 yaliyotumika kuwashambulia askari yamedhibitika kutoka kwenye bunduki iliyokutwa eneo la tukio.

Hata hivyo, Kamanda Malimi ametoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi pale ambapo wataona kikundi cha watu ambao wanawatilia mashaka kutoa taarifa kwa jeshi la polisi ili kufanya uchunguzi kabla ya  uhalifu haujajitokeza.

 

 

Katibu Mkuu Chadema ampongeza Maalim Seif
Askari watiwa mbaroni kwa kumchapa vibao dereva, Masauni athibitisha

Comments

comments