Mabingwa wa kombe la Shirikisho Tanzania bara (ASFC) Azam FC, wanaamini bado wana kikosi bora na chenye ushindani, licha ya kutochukua ubingwa kwa misimu sita mfululizo.

Afisa Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo yenye maskani yake Azam Complex, Chamazi jijini Dar es salaam,  Abdulkarim Amin ‘Popat’ amesema kikosi chao bado kinatoa ushindani, na bado kipo kwenye mbio za kuwania ubingwa kwa kuwa hawajatoka ndani ya nafasi tatu za juu.

“Timu ikiwa kwenye nafasi tatu za juu ina maana kwamba, bado ipo kwenye harakati za kunyakua ubingwa, lakini shida ni kwamba hatujabahatika tu kuchukua ubingwa.

“Ni kweli tumeyumba katika kipindi hiki cha Corona, kama unavyojua kulikuwa hakuna kitu chochote kilichokuwa kinaendelea na timu yetu sisi ni timu ya kampuni, na  inategemea kampuni zake inavyojiendesha.

“Kwa hapa ndani shughuli zilikuwa zinaendelea, lakini huko nje mambo yalisimama kutokana na nchi nyingi mipaka yake kufungwa.”

Alisisitiza kuwa, “Kikubwa tulichoathirika katika kipindi hicho ilikuwa ni kucheza mechi za nyumbani nje ya uwanja wa nyumbani, na kabla ya hapo tulikuwa na rekodi nzuri hapa nyumbani, lakini baada ya kutoka hapa tulipoteza mbele ya Coastal Union na kutoa droo kama mbili, kwaiyo hiyo ndio athari tuliyoipata.” Azam FC inashika nafasi ya pili na pointi 54.

Ripoti kifo cha George Floyd zatofautiana, Serikali yadai ‘alikuwa anaumwa’, wataalamu waja na yao
Waziri Mkuu atangaza mapinduzi zao la Mkonge Tanzania