Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameialika timu ya Young Africans S.C. (Wananchi) kula nae chakula cha jioni Ikulu Dar Es Salaam kesho Juni 5, 2023 mara baada ya mchezo wa fainali kati ya USM Alger uliochezwa juni 3, 2023 huko Algiers.

Hayo yamesemwa na Msemaji mkuu wa Serikali Gerson Msigwa leo June 4, 2023 kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo amewapongeza Yanga kwa kupata ushindi wa goli moja kwa sifuri dhidi ya mpinzani wao USM Alger.

”Ni kweli tulitarajia tungepata ubingwa wa Kombe la Shirikisho katika pambano hili lakini mpira ndivyo ulivyo kwa mwanamichezo yeyote atakubaliana nami kwamba Yanga jana wameonyesha uwezo na kwamba Young Africans inatoka Tanzania uwakilishi mzuri kule Algeria leo kila kuinga inazungumzwa Yanga na jinsi ambavyo wameonyesha mchezo mkubwa katika fainali” amesema Msingwa

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Juni 5, 2023
Watu 25 wahofiwa kunywa pombe yenye sumu Songwe