Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za pole kwa wanahabari na wafiwa wote kutokana na ajali iliyotokea leo katika eneo la Nyamikoma wilaya ya Busega Mkoani Simiyu na kusababisha vifo vya watu 14 wakiwamo waandishi wa habari sita.

Rais Samia ametuma salama hizo leo Jumaane Januari 11, 2022 ambapo amesema amestushwa na vifo hivyo vilivyotokea baada ya gari ya waandishi wa habari waliokuwa kwenye msafara wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza (RC), Robert Gabriel kugongana na gari ya abiria aina ya Toyota Hiace .

“Nimeshtushwa na vifo vya Watu 14 wakiwemo Wanahabari 6 vilivyotokea leo asubuhi baada ya gari lililokuwa katika msafara wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kugonga na Daladala. Poleni Wafiwa, Wanahabari na jamaa wote. Mungu aziweke mahali pema roho za Marehemu na Majeruhi wapone haraka”ameandika kupitia ukuraa wake wa Tweeter

Mkuu wa Wilaya ya Busega (DC), Gabriel Zakaria amethibitisha kutokea vifo vya watu 14 ambapo 11 walifariki papo hapo huku wengine watatu wakifariki muda mfupi baada ya ajali hiyo kutokea.


Alisema katika vifo hivyo kuna vifo vya waandishi wa habari wanne na dereva wao na watu wengine sita waliofariki papo hapo.

“Ni kweli ajali hiyo imetokea, watu 11 wamefariki kwenye eneo la tukio wakiwemo waandishi wa habari wanne na dereva na wengine sita waliokuwa kwenye gari lingine” alisema Zakaria na kuongeza.

Binti aliyemuua mama yake alitaka pesa za mafao
Breaking News: Waandishi wa Habari wafariki ajalini Simiyu