Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo amesema ilani ya uchaguzi ya chama hicho ya mwaka 2020/25 imebeba ajenda ya kilimo kama kipaumbele kikuu cha malengo ya kuleta mapinduzi nchini kupitia sekta hiyo.

Ametoa kauli hiyo leo Agosti 8, 2022 alipokuwa akizungumza katika kilele cha maadhimisho ya sikukuu ya wakulima kilichofanyika mkoani Mbeya.

Amesema, “Malengo ya wizara yamejielekeza kwenye kuikuza sekta hii kufikia asilimia 10 ya kuchangia uchumi wa nchi ifikapo 2030.”

Aidha Chongolo, amempongeza Rais Samia kwa kusimama na wakulima wa nchi hii bada ya kuzindua mfumo wa Ruzuku za pembejeo za kilimo hasa mbolea.

“Zaidi ya bilioni 150 za kitanzania na dola milioni 77 za Marekani umezipeleka kuhahakisha zinachangia kupunguza mzigo wa pembejeo na hasa mbolea kwa wakulima nchini.” amesema Chongolo

Serikali yasema haitavumilia ukatili, biashara ya Binadamu
Wakulima waaswa kuzingatia kilimo chenye tija