Ule msemo wa Wahenga kuwa ‘wagombanao ndio wapatanao’ umedhihirika tena leo baada ya mkali wa RnB, Rama Dee kumalizana rasmi na kituo cha redio cha Clouds Fm ikiwa ni miaka kadhaa tangu ashiriki harakati za Anti-Virus dhidi ya kituo hicho.

Rama Dee ambaye alikuwa kwenye XXL ya Clouds Fm kwa ajili ya kutambulisha wimbo wake mpya ‘Nibebe’ alieleza kuwa alishiriki kwenye kanda mseto za Anti-Virus kwa sababu na ameamua kurudi nyuma na kupatana na kituo hicho kwa sababu bora zaidi.

“Mimi nasema kwa mashabiki wangu wote wanaonisikiliza, sasa hivi ni muda wa sisi kukaa pamoja. Kwahiyo, kwa chochote ambacho kiliwahi kutokea kwa Rama Dee ambacho kilionekana sio sahihi, naweza kusema ‘I’m sorry’ kwa Clouds Fm wenyewe,” alifunguka.

“Na kama [Clouds Fm] wanaona kuna sehemu walinikosea tayari tumeshazungumza nao na tumeshamaliza,” ameongeza.

Rama Dee ambaye aling’arisha viitikio vingi kwenye Anti-Virus iliyolenga kuishambulia kwa maneno Clouds FM amekuwa msanii wa tatu kutoka kwenye harakati hizo kujitokeza hadharani na kutangaza kuweka kando harakati hizo.

Hata hivyo, Mkali huyo alieleza kuwa lengo halisi la Anti-Virus lilikuwa kueleza matatizo katika masuala yote ya kijamii, siasa na megine lakini baada ya wajumbe wengine kuongezeka walikuja na mizuka yao na ndipo vita ya maneno dhidi ya Clouds Fm iliposhika hatamu.

Wa kwanza kushikana mikono ya amani na Clouds alikuwa Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph ‘Sugu’ Mbilinyi ambaye alikuwa akiongoza harakati hizo, kisha wasanii wawili mapacha wa Pasu Kwa Pasu na leo Rama Dee ameunga msafara wa amani
Sikiliza wimbo wake mpya hapa, ‘Nibebe’:

Said Mrisho: Nimeachana na mke wangu ila sijatelekeza familia
TRA yaifungia Radio Free Africa (RFA)