Klabu ya Real Madrid imethibitisha kumuuza mshambuliaji wake Cristiano Ronaldo kwenda Klabu ya Juventus ya Italia kwa dau la Euro Milioni 105 sawa na takribani Tsh. 280,544,600,000

Ronaldo anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka minne na ‘bibi kizee huyo wa Turin’ ambao utagharimu Euro Milioni 30(takribani Tsh. 80,106,930,000) kwa mwaka

Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa na klabu ya Real Madrid imetangaza kuwa, kwa mujibu wa matakwa na maombi yaliyotolewa na Ronaldo, imekubali kumuuza kwenda klabu ya Juventus

Aidha, klabu hiyo imemshukuru mchezaji huyo ambaye anatambulika kuwa moja ya wachezaji bora dunia kwa miaka yote 9 aliyokaa klabuni hapo

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Julai 11, 2018
CCM yamsimamisha Christopher Chiza kugombea jimbo la Kasuku Bilago

Comments

comments