Aliyekua mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya shirikisho la soka nchini TFF Revocatus Kuuli amefungiwa kujihusisha na soka maisha, baada ya kesi yake kujadiliwa na kutolewa maamuzi na kamati ya maadili ya shirikisho hilo.

Mwenyekiti wa kamati ya maadili Hamidu Mbwezeleni, mapema hii leo alizungumza na waandishi wa habari na kusoma hukumu ya Kuuli, ambaye alifikishwa mbele ya kamati hiyo kufuatia sakata lake na katibu mkuu wa TFF Wifred Kidau, ambaye alimuandikia barua ya kutoa maelezo ya kuingilia uchaguzi mkuu wa klabu ya Simba.

Mbwezeleni amesema baada ya Kuuli kuandikiwa barua hiyo na katibu mkuu wa TFF, alifanya makosa ya kimaadili kwa kuisambaza katika mitandao ya kijamii, kwa makusudi yake binafsi.

Kuuli amefungiwa kufuatia sakata la uchaguzi Simba ambapo alihojiwa kwanini ameamua kuuzuia mchakato wake kipindi unaanza na kupewa siku tatu kwa ajili ya kutoa majibu.

Wakati huo huo Kamati ya Uchaguzi ya TFF imetangaza kuanza mchakato wa uchaguzi maalum wa kujaza nafasi ambazo zilizo wazi ndani ya klabunya Young Africans  ikiwemo ile ya Mwenyekiti.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Ally Mchungahela amesema zoezi la kuchukua fomu kwa wagombea litaanza Novemba 8 hadi 13 2018, huku uchaguzi huo ukitarajiwa kufanyika Januari 13 2019.

Kamati ya uchaguzi ya TFF imetangaza rasmi kuanza mchakato huo mara baada ya Baraza la Michezo Tanzania (BMT) kuwataka wausimamie wakieleza kuwa kamati ya Yanga haijitoshelezi.

BMT waliitaka TFF itimize majukumu hayo katika kikao na wanahabari kilichofanyika siku chache zilizopita.

Mayweather kuzichapa na bingwa wa Kickboxing Japan
Muro aanza kuwashughulikia vigogo waliopiga bilioni 3 za Kanisa

Comments

comments