Timu ya taifa ya Romania itacheza bila la mashabiki katika mchezo dhidi ya Lithuania mwezi ujao, baada ya kuthibitika mashabiki wa soka wa nchi hiyo, walionyesha vitendo vya ubaguzi wa rangi wakati wa mchezo dhidi ya Serbia uliochezwa mwezi huu.

Shirikisho la soka barani Ulaya (UEFA), limetoa taarifa ya adhabu kwa timu ya taifa ya Romania, bada ya kupitia ripoti zilizowasilishwa na msimamizi wa mchezo dhidi ya Serbia, uliomalizika kwa sare ya bila kufungana.

Mbali na timu ya taifa ya Romania kupewa adhabu ya kucheza bila mashabiki, shirikisho la soka barani Ulaya UEFA limekitoza chama cha soka nchini humo faini ya Euro 50,000 sawa na dola za kimarekani 56,835, kwa kosa la ubaguzi wa rangi ulioonyeshwa na mashabiki wao.

UEFA pia imekitoza chama cha soka nchini Romania faini ya Euro 23,000, kwa kosa la kushindwa kudhibiti vitendo vya kibaguzi.

Timu ya taifa ya Romania itakua mwenyeji wa Lithuania Novemba 17, katika mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi ya michuano ya UEFA Nations League.

Sakata la vilipuzi nchini Marekani bado kitendawili
Makonda amvutia kasi Amber Rutty, amtaka ajisalimishe polisi

Comments

comments