Bodi ya Ligi, imethibitisha kupokea rufaa ya Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans, inayopinga suala la wachezaji wa Mbeya City kuzidi Uwanjani, wakati wa mchezo wa ligi kuu uliochezwa mwishoni mwa juma lililopita mjini Mbeya.

Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya ligi, Boniface Wambura Mgoyo, amethibitisha kuwa rufaa hiyo imewafikia na tayari imeshawasilishwa mahala husika.

Young Africans waliwasilisha rufaa yao saa kadhaa baada ya mchezo dhidi ya Mbeya City, uliomalizika kwa sare ya bao moja kwa mojakatika Uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine.

Wakati huo huo Katibu Mkuu wa Young Africans Charles Boniface Mkwasa, ameitaka bodi ya ligi kuichukua hatua za kinidhamu Mbeya City FC baada ya mashabiki wake kufanya vurugu wakati wa dhidi yao.

Mchezo huo uliounguruma siku ya jumapili ulilazimika kusimama kwa dakika 4 kipindi cha pili baada ya mashabiki wa Mbeya City kuanzisha vurugu na kufikia hatua ya kurusha mawe Uwanjani.

Vurugu za mashabiki wa Mbeya City zilizuka baada ya Young Africans kuandika bao la kwanza kupitia kwa Raphael Daud Alpha.

Mbali na mashabiki kufanya fujo, Mkwasa amesema bodi ya ligi inapaswa kuiadhibu Mbeya City kufuatia kitendo cha kuzidisha wachezaji Uwanjani ilihali tayari mmoja wao alikuwa ameshatolewa nje kwa kadi nyekundu.

Ufaransa yampoteza Henri Michel
Per Mertesacker: Tukitwaa Europa League itakua heshima kwa Wenger

Comments

comments