Jeshi la Polisi nchini Nigeria, linawashikilia Vijana saba wanaotuhumiwa kumbaka msichana mwenye umri wa miaka 15 katika kijiji cha Kodomun, eneo la Serikali ya Mtaa ya Demsa uliopo Jimbo la Adamawa.

Msemaji wa Polisi wa Jimbo hilo, SP. Suleiman Yahaya katika taarifa yake alisema vijana hao kupitia mmoja ambaye ni mpenzi wake walimrubuni mwathiriwa na kumpeleka nyumbani kwa mpenzi wake na kumbaka kwa nguvu.

Vijana hao saba ambao wanatuhumiwa kumbaka msichana wa umri wa miaka 15 kwa zamu.

Amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Ephraim Emmanuel (17), Madapwa Fidelis,17, Paka Albert (16), Jude Shido Aventi (18), Harmony Manade (18), Napwanwa Nahim Edmanth (16) na Manbiah Ojes (16), wote wakiwa ni wakazi wa kijiji cha Kodomun.

Kufuatia tukio hilo, Kamishna wa Polisi, CP Afolabi Babatola amemuagiza Naibu Kamishna wa Polisi anayeshughulikia Upelelezi wa Makosa ya Jinai (CID), kufanya uchunguzi huku akiwashauri wazazi kuwa waangalifu na watoto wao hasa wa kike.

Tanzania Prisons kamili kuivaa Namungo FC
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Machi 9, 2023