Sakata la Ununuzi wa Korosho limeendelea kuwasha moto bungeni baada ya Mbunge wa Mchinga (CUF), Hamidu Bobali kusema yupo tayari kujiuzulu ubunge iwapo itathibitika kwamba wakulima hawalipwi Sh2,640 kwa kilo badala ya Sh3,300 iliyotangazwa na Rais Dkt. John Magufuli.
 
Akichangia taarifa ya Kamati za Bunge ya Bajeti na Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC), Bobali ameitaka Serikali kueleza kama itaendelea kuwalipa wakulima wa Korosho daraja la kwanza kwa Sh3,500.
 
“Tunataka kauli kama mmeuza kwa Sh4,180 hii iliyozidi mtawarudishia wakulima? Jambo la pili, hivi sasa ninavyozungumza wakulima wanalipwa Sh2,640 kwa kilo ya korosho sio tena Sh3,300,” amesema Bobali
 
Aidha, Rais Dkt. Magufuli alitangaza kuwa wakulima watalipwa Sh3,300 kwa kila kilo ya Korosho watakayoiuzia Serikali na hakuna kauli iliyotolewa kubatilisha agizo hilo.
 
Hoja ya mbunge huyo ilimfanya Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Stella Manyanya kusimama akitumia kanuni ya 64 A na kusema kuwa Bobali amelidanganya Bunge, ambapo kauli hiyo ilizua kelele kwa baadhi ya wabunge kupinga kwamba kanuni hiyo iliyotumiwa na Manyanya haipo kwenye Kanuni za Bunge hali iliyomfanya Spika amruhusu Bobali kuendelea na kuchangia hoja yake.
 
Akijibu hoja hiyo, Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga amesema kuwa kumekuwa na taarifa za upotoshaji juu ya bei ambayo Serikali inanunulia Korosho.
Hata hivyo, Hasunga ameongeza kuwa ukijumulisha ushuru (Export levy) ambao ni Sh360, kilo moja ya Korosho inakuwa imeuzwa kwa zaidi ya Sh4,160 kwa kilo, ambapo hadi sasa, Serikali imeuza tani 100,000 za Korosho na wanaendelea kuuza na kwamba, wakishawalipa watu wote watafahamu wamepata faida kiasi gani.
  • Njombe bado hali tete mauaji ya watoto
 
  • Benki ya Dunia yatoa Bilioni 21.7 kuboresha miundombinu Mtwara
  • Video: Malima awasha moto sakata la Diwani kukunja nne kikaoni
 

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Februari 4, 2019
Tukumbushane tafsiri 4 za kumpa mwenza wako zawadi