Mshambuliaji wa pembeni kutoka nchini Misri Mohamed Salah amepita katika vipimo vya afya na wakati wowote kuanzia sasa atasaini mkataba wa kuwatumikia majogoo wa jiji Liverpool akitokea AS Roma ya Italia.

Salah aliwasili Merseyside jana usiku, na mapema hii leo alianza kufanyiwa vipimo vya afya huku ada yake ya usajili ikipunguzwa kutoka Pauni Milioni 40 hadi milioni 34.

Mtandao wa gazeti la The Sun umeandika kuwa, mshambuliaji huyo atasaini mkataba wa miaka mitano na atakua analipwa mshahara wa Pauni elfu 90 kwa juma.

Salah anakaribia kuondoka AS Roma huku akiacha kumbukumbu ya kufunga mabao 19 msimu uliopita na kutoa pasi za mwisho 12.

JPM ampa mtihani mwingine Mwijage
?Live: Hotuba ya Rais Magufuli katika uzinduzi barabara ya Bagamoyo - Msata