Timu ya Taifa chini ya miaka 16 Serengeti Boys inaendelea kujiandaa na mashindano ya CECAFA kwa vijana yatakayofanyika Burundi.

Kikosi hicho kipo kambini kwenye hostel za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF,Karume-Ilala,Dar es Salaam.

Mashindano hayo ya CECAFA kwa Vijana yataanza April 1 mpaka April 15 huko Burundi.

wakati huo huo timu ya Taifa ya Vijana wenye umri chini ya miaka 13 (U13) inatarajiwa kushiriki michuano ya vijana itakayozikutanisha timu za vijana za nchi zaidi ya 10 kutoka mataifa mbalimbali yatakayofanyika nchini Ubelgiji mwezi Agosti, 2018.

TFF inaandaa utaratibu sahihi wa kupata kikosi cha timu ya Taifa kwa vijana wenye umri huo ili kuweza kujiandaa na michuano hiyo ya vijana.

Kwa kuanzia kutachezwa mechi kati ya vijana wenye umri chini ya miaka 13 kutoka Tanzania Bara dhidi ya vijana wa Zanzibar katika siku za hivi karibuni ili kutoa nafasi kwa waalimu kuchaguwa wachezaji wenye vipaji watakaounda kikosi hicho cha U13.

Robo fainali kombe la shirikisho (ASFC)
Ngorogoro Heroes kujipima kwa Morocco, Msumbiji

Comments

comments