Wizara ya Maliasili na Utalii  imesema kuwa italipa madeni yote ya miaka ya nyuma na vifuta jasho inayodaiwa na wananchi waliopata uharibifu wa wanyamapori nchini kabla ya bunge lijalo la bajeti.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Ramo Makani wakati wa kuhitimisha ziara yake ya siku moja ya kufuatilia matatizo ya uhifadhi wilaya ya Bunda.

Makani amesema uamuzi huo wa Serikali utaondoa kilio cha muda mrefu cha wananchi ambao wamepata madhara mbalimbali ya wanyamapori ikiwemo vifo,majeruhi,mazao kuliwa na kuharibiwa mashamba yao.

“Serikali ya awamu ya tano imeshakamilisha takwimu za madai, yale yote tunayodaiwa huko nyuma,yaliyoifikia wizara yamehakikiwa”amesema Makani.

Hata hivyo amsema kuwa wilaya nyingi zilizoathirika zaidi na vitendo hivyo ambazo madai yao ni makubwa zaidi ya zingine ni Serengeti na Bunda ambazo ziko mkoani Mara na zinapakana na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

Zitto kabwe avunja ukimya
Ndikilo awapa siku 30 wafugaji kuondoa mifugo yao