Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema Tanzania inatarajia kupokea Dozi Milioni 2 za Sinopharm kutoka Nchini China za kujikinga na ugonjwa wa Uviko-19

Amesema hayo wakati akizumgumza na waandishi wa habari mkoani Singida wakati akitoa tarifa ya wiki ya Serikali.

“Tunatarajia mwanzoni mwa mwezi ujao chanjo nyingine dozi Milioni 2 kutoka nchini China (SINOPHARM) zitafika nchini ili Watanzania waendelee kupata chanjo bila matatizo”amesema Msigwa

“Kwa kutambua kuwa chanjo zinaweza kuisha muda wowote kuanzia sasa, Serikali inakamilisha utaratibu wa kuleta chanjo nyingine dozi Milioni 2 kutoka nchini China (SINOPHARM) “amesema Msigwa

Msigwa pia amewasihi wale ambao hawependi kuchoma sindano kuchangamkia dozi ya Janssen ambayo unachoma mara moja tu.

“Nawasihi wale ambao hawapendi kuchoma sindano mara mbili kuchoma chan zilizopo sasa kabla hazijaisha kwa sababu chanjo zinazotolewa sasa ni aina ya JANSSEN (JJ) kutoka Marekani, chanjo hizi unachoma mara moja tu na unapata kinga ya mwaka mzima”.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Septemba 27, 2021
Maziwa ya nyuki yanaongeza nguvu za kiume