Serikali imesema, makusanyo ya tozo ya miamala yameiwezesha Serikali yamekuwa yakitoa huduma za msingi za Wananchi katika mwaka wa fedha 2021/22, ambapo Serikali ilitumia jumla shilingi bilioni 7 zilitokana na tozo ya miamala kwa ajili kujenga madarasa.

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba ameyasema hayo Bungeni jijini Dodoma hii leo Septemba 20, 2022 na kudai kuwa Serikali ilitumia jumla ya shilingi bilioni 143.7 kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya afya na kati ya fedha hizo, shilingi bilioni 117 sawa na asilimia 81.4 ya fedha zote, zilitokana na tozo ya miamala.

Amesema, “Serikali ilitumia jumla ya shilingi bilioni 611.3 kwa ajili ya mikopo ya elimu ya juu na kati ya fedha hizo, shilingi bilioni 221.3
zilitokana na tozo huku na kwa upande wa TARURA, Serikali ilitumia jumla ya shilingi bilioni 735.7 kwa ajili ya ujenzi wa barabara vijijini.

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba.

Waziri Nchema ameongeza kuwa, kati ya kiasi hicho shilingi bilioni 13.5 zilitokana na tozo kwenye miamala na kiasi kingine ni tozo kwenye mafuta na kwamba katika mwaka wa fedha 2022/23, kulikuwa na mahitaji muhimu na ya lazima, ambayo yangeweza kukosa fedha kutokana na ufinyu wa bajeti.

“Baadhi ya masuala muhimu ambayo yangeathiriwa kama tungefuta kabisa chanzo hiki ni (a) tungeelekeza fedha za mkopo wa ECF kwenye madarasa mwaka huu, tusingeweza kupeleka bilioni 954 kwenye kilimo zinazolenga kujenga miundombinu ya umwagiliaji, mbegu bora pamoja na block farming,” amefafanua Mwigulu.

Aidha ameongeza kuwa, “Serikali ilitumia busara ya kiuchumi kupeleka fedha hizo kwenye sekta za uzalishaji ili kutengeneza ajira kwa vijana, na fedha za kutoa huduma za jamii zitafutwe kutoka kwenye tozo na tusingeweza kupeleka bilioni 145 kwenye mifugo, uvuvi, kununua boti za uvuvi, kuchochea ukuaji sekta ya mifugo na kujenga miundombinu na mitaji kwa wamachinga.

Mataifa 'yalegeza kamba' vita ya njaa na utapiamlo
Viongozi wakutana kujadili hali ya kutoaminiana