Serikali nchini, imesema imeondoa ukomo wa matumizi ya vitambulisho vya Taifa vilivyoisha muda wake, huku ikizitaka taasisi zote na kampuni kuendelea kuvitambua vitambulisho hivyo.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni jijini Dar es Salaam na kuongeza kuwa Serikali imefanya mabadiliko ya kikanuni ya utambuzi na usajili ili kuruhusu kuondoa ukomo wa matumizi wa Vitambulisho hivyo.

Amesema, “watoa huduma kwa Wananchi hasa taasisi za kifedha, Benki na Kampuni za simu ziendelea kuvitambua na kuvitumia vitambulisho vya Taifa vyenye tarehe ya ukomo kwa sababu havitakuwa na ukomo wa matumizi tena.”

Aidha, Waziri Madauni amefafanua kuwa, marekebisho hayo hayatahusha vitambulisho vya wageni wakazi na wakimbizi na tayari kanuni hizo zimeanza kutumika baada ya tangazo rasmi la serikali (GN) Na 96 la Februari 17, 2023.

Putin alikosea kudhani ataishinda Ukraine: Biden
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Februari 22, 2023