Licha ya kuomba msamaha Msanii wa filamu nchini Tanzania, Wema Sepetu leo ameitwa kuhojiwa na Bodi ya Filamu Tanzania baada ya kusambaa kwa video ya faragha katika mitandao ya kijamii.

Akizungumza na kituo cha Televisheni cha EATV, Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza amesema kuwa wameanza kuwachukulia hatua wasanii wote ambao wanatumia mitandao ya kijamii vibaya na wanao chapisha video zenye maudhui ya ngono mitandaoni

Shonza amesema kuwa licha ya wasanii hao kuhojiwa na Bodi ya filamu pia watahojiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Kambi ya Taifa Stars yapangua tena ratiba ligi kuu
Alexander Hleb: Nilifanya makosa kuondoka Arsenal

Comments

comments