Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amezindua mradi wa ghala la kuhifadhi mazao ya chakula katika kijiji cha Ikindilo kilichopo Wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu, ambao unalenga kudhibiti sumukuvu kwenye mazao ya chakula, unaofadhiliwa na GAFSP, Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) na Serikali Kuu..

Majaliwa amefanya uzinduzi huo Machi 24, 2023 Kijijini hapo na kupokea taarifa toka kwa Meneja wa mradi huo, Eng. Mohamed Kombo ambaye alisema ujenzi wa ghala hilo na miundombinu yake, ulianza Agosti 9, 2021 na kukamilika Februari 15, 2023.

Amesema, “Lengo la mradi huu ni kusaidia kutoa elimu ya uhifadhi na kudhibiti sumukuvu kwenye mazao ya chakula ili kupunguza madhara yatokanayo na utumiaji wa mazao yaliyochafuliwa na kuvu inayosababisha sumukuvu, tayari ujenzi umekamilika kwa asilimia 100, na mkandarasi amekwishakabidhi mradi kwa Halmashauri na kuanza kipindi cha uangalizi (defect liability period) cha mwaka mmoja.”

Wizara ya Kilimo kupitia mradi wa TANIPAC ipo katika hatua za mwisho za ununuzi ya vifaa vya ghala na maabara, ikiwemo chaga za kuhifadhia magunia, mashine ya kupima sumukuvu, mashine ya kupima unyevu, komputa ya mezani na mizani na vifaa hivyo vinatarajiwa kufikishwa kwenye mradi Mei, mwishoni.

Ligi ya Championship kurushwa Live
Ofisi ya Makamu wa Rais kuanzisha kituo nyaraka za Muungano