Fainali ya kombe la SportPesa Super Cup 2018 inatarajiwa kupigwa leo ambapo mabingwa wa Tanzania Simba SC watachuana na klabu ya Gor Mahia ya Kenya mchezo utakaopigwa majira ya saa 9 Alasili katika dimba la Afraha mjini Nakuru nchini Kenya.

Simba SC imefika fainali baada ya kuzitoa Kariobangi Sharks ya Kenya kwa penati 3-2 na Kakamega Homeboys ya Kenya kwa penati 5-4 baada ya sare ya 0-0 ndani ya dakika 90 katika michezo yote miwili.

Kwa upande wa Gor Mahia wamefika fainali kwa kuzichapa JKU  ya Zanzibar kwa mabao 3-0 na kuipiga Singida United ya Tanzania Bara kwa mabao 2-0.

Bingwa wa SportPesa Super Cup atapata kitita cha dola za Kimarekani 30,000 pamoja na nafasi ya kwenda kucheza na klabu ya Everton katika uwanja wa Goodison Park mjini Liverpool, England wakati mshindi wa pili akitarajia kupata dola za Kimarekani 10,000.

Mshindi wa tatu atapata dola 7, 500 na wa nne dola 5,000 wakati timu nyingine zitapewa kifuta jasho cha dola 2,500. Gor Mahia ndiye bingwa mtetezi ambaye mwaka jana iliifunga AFC Leopards 2-1 katika fainali iliyopigwa uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Hatima ya Yanga kujulikana leo
Samia Suluhu aishika mkono Hospitali ya Mloganzila