Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo – CHADEMA, Tundu Lissu mesema hana kinyongo na yeyote na tayari amesahau kila lililotokea kuhusiana na tukio lililompata Septemba 7, 2017 kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana jijini Dodoma.

Lisu ameyasema hayo hii leo Februari 4, 2023 jijini Dar es Salaam wakati akifanya mahojiano maalum na Dar24 Media na kudai kuwa japo waliompiga risasi wanafahamika lakini hiyo haimfanyi kuendelea kuishi kwa kinyongo bali amekaribisha maisha mapya.

Amesema, “walionipiga risasi ambao wanaitwa wasiojulikana wapo na wanafahamika mimi ninawaita wanaojulikana lakini nimesamehe na sina kinyongo na yeyote na nimekaribisha maisha mapya lazima maisha yaendelee.”

Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lisu wakati akifanya mahojiano maalum na Dar24 Media nyumbani kwake.

Aidha Lisu ameongeza kuwa japo kumbukumbu zitaendelea kubaki kuhusiana na tukio hilo lakini kamwe hataishi kwa kubakia hapo na badala yake anangalia ni namna gani ataendelea kuishi ili kutimiza azma ya kulikomboa Taifa kwa njia zinazofaa kupitia siasa.

“Ukinitazama mwili wangu sehemu nilizojeruhiwa huwezi kudhani kama ni kweli nimepona, mwili mzima una ramani za operesheni za madaktari na waliniambia huu ni muujiza maana ka damu niliyopoteza siku ya tukio sikupaswa kuendelea kuishi lakini leo niliyepigwa risasi mwili mzima bado ninaishi.”

Hata hivyo, Lisu amesema kilichomtokea mpaka kuendelea kuishi hii leo ni muujiza wa MUNGU na kwamba licha ya maombi ya wananchi wenye mapenzi mema na ibada alizofanya nyumbani kwao Ikungi Mkoani Singida tukio hilo ni ushuhuda tosha kuwa yale yaliyoandikwa juu ya miujiza katika Biblia, leo yamejidhihirisha wazi.

Ilamfya awashangaa wanaomshangaa
Neymar kuondoka Paris Saint-Germain