Timu ya Singida United imepania kufanya makubwa katika Ligi Kuu msimu ujao mara baada ya kumsajili mkali wa kufumania nyavu kutoka nchini Rwanda ambaye alikuwa akiichezea timu ya Polisi nchini humo, Danny Usengimana na kukamilisha idadi ya wachezaji sita wa kigeni ambao imewasajili kwaajili ya msimu ujao.

Aidha, Mshambuliaji huyo anatabiliwa kuwa tishio katika kufumani nyavu ukanda wa Afrika Mashariki na Kati ambapo ameingia mkataba wa miaka miwili na kikosi cha Kocha wa zamani wa mabingwa Ligi Kuu ya Tanzania bara Yanga ,Hans Van Der Pluijm.

Hata hivyo, Singida United ni miongoni mwa timu tatu zilizopanda kushiriki michuano ya ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara huku nyingine zilizopanda ni Lipuli ya Iringa pamoja na Njombe Mji.

Moto mkubwa wasababisha vifo vya watu 25
Sylvester ‘Rambo’ adai Mayweather atapata kesi ya mauaji akipigana na McGregory

Comments

comments