Stamina aka Kabwela amekuwa msanii wa kwanza wa hip hop kueleza kuwa atafuata ushauri wa Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe wa kutoimba kuhusu masuala ya siasa.

Stamina ambaye alitambulisha rasmi video yake ya wimbo mpya ‘Bora Tuoane’ kwenye Friday Night Live ya East Africa Radio Ijumaa iliyopita, alisema kuwa hivi sasa amebadilika huku akiwashauri wasanii wengine kuisikiliza Serikali kuhusu kuachana na nyimbo za siasa.

“Ni vizuri kuisikiliza serikali… mtu mmoja huwezi kushindana na serikali,” alisema Stamina. “Kwanza hakuna mwana harakati ambaye yuko hai, wanaharakati wote wameshakufa (aliongeza na kuangua kicheko kwa utani),” aliongeza.

VIDEO: G Nako, C Pwaa watajwa awamu ya pili Kanjubahi

Rapa huyo aliwataka mashabiki waendelee kumuunga mkono kwani mwaka huu ni mwaka wa mabadiliko makubwa kwenye muziki wake.

Alisema kuwa hivi sasa yuko chini ya menejimenti mpya na kwamba meneja anayemshika mkono ni mtayarishaji wa muzi wa A.M Records, Manecky. Alitamba kuwa kutokana na kuwa na usimamizi mzuri wa kazi zake, wameazimia kuachia wimbo mpya na video kila baada ya mwezi mmoja.

VIDEO: Ni Noma! Wakazi, Zaidi, P The MC baada ya kutambulisha ngoma yao mpya wafunguka mengi

Nicki Minaj Awaokoa Wanawake wa Kijiji cha India
Snoop Dogg Ageukia Muziki wa Injili, Ajipanga Kuachia Albam Ya ‘Upako’