Siku moja baada ya kutangazwa kuwa meneja wa kikosi cha Inter Milan, Stefano Pioli ameeleza wazi hisia zake kwa klabu hiyo ya mjini Milan kwa kusema ni shabiki mkubwa wa The Nerazzurri.

Pioli amezungumza suala hilo alipokutana na waandishi wa habari kwa mara ya kwanza tangu alipotangazwa kuwa mkuu wa benchi la ufundi klabuni hapo.

Amesema huenda wadau wengi wa soka walikua hawafahamu ni vipi anavyoipenda Inter Milan, lakini ukweli ni kwamba pamoja na kuwahi kufanya kazi katika klabu nyingine bado aliipenda klabu hiyo yenye historia kubwa nchini Italia.

Babu huyo mwenye umri wa miaka 51 ameongeza kuwa, hatua ya kupata ajira katika klabu anayoipenda anaamini itamsaidizi kufanya kazi kwa uweledi mkubwa na kufikia malengo yanayokusudiwa.

Kuhusu mchezo wa mwishoni mwa juma lijalo ambao utakua wa kwanza kwake kama mkuu wa benchi la Ufundi, Pioli amesema kutakua na changamoto kubwa dhidi ya Bologna, lakini atajitahidi kufanya mipango ya kukiandaa vizuri kikosi chake ili kufanikisha azma ya kuzinyakua point tatu muhimu.

Pioli amewahi kufanya kazi na timu ya vijana ya Bologna (1999–2002), timu ya vijana ya Chievo (2002–2003), Salernitana (2003–2004), Modena (2004–2006), Parma (2006–2007), Grosseto (2007–2008), Piacenza (2008–2009), Sassuolo (2009–2010), Chievo (2010–2011), Palermo (2011), Bologna (2011–2014) na Lazio (2014–2016)

Twiga Stars Kuwapima Wenyeji Wa Fainali Za Afrika 2016
Sergio Kun Aguero: Sina Ugomvi Na Pep Guardiola