Mwanamuziki mkongwe wa bongo fleva maarufu kama TID anayetamba na wimbo wake mpya aliomshirikisha mkongwe Lady Jay Dee unaoenda kwa jina  la ‘any more’ amemaliza bifu lake na kisoka ambaye aligombanana naye miezi minne iliyopita.

Wawili hao walitofautiana hadi kufikia hatua ya kuumizana usoni  lakini amabpo TID kupitia ukurasa wake wa instagram kwa hivi sasa ameonekana kumaliza tofauti zao baada ya kupiga picha wakiwa pamoja wakicheka hali iliyoashiria wako sawa.

Aidha kwa upande wa TID amesema sasa hivi hana tofauti wala bifu tena na jamaa huyo na kukataa kuweka wazi ilikuwaje hadi wamemaliza tofauti zao.

“Tumemaliza tofauti zetu, hatuna tena bifu hatutaki kurudi nyuma, tunatakiwa kwenda mbele kama tuligombana na kupishana kauli kwa kuwa tulikuwa tumelewa kwanini tuendelee kugombana na kutishiana”

Sisi ni kizazi cha amani cha Tanzania ni mfano tunawashawishi hadi watu wa nchi za nje kufanya muziki na sisi kwahiyo tumekuwa ni mfano mzuri na tunatakiwa kubaki hivyo, siwezi kutoa details zaidi ila yameisha ” amese T.I.D

Rais Magufuli amteua Kichere kuwa CAG, ajaza nafasi ya Prof. Assad
Kijana aliyeishi na vidole 9 kwenye mguu mmoja atimiza nadhiri yake

Comments

comments