Timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) itacheza mchezo wake wa kwanza wa Kufuzu fainali za Mataifa Bingwa Barani Afrika (CHAN) dhidi ya Rwanda, katika Dimba la CCM Kirumba Jijini Mwanza.

Afisa Habari wa Shirikisho la Soka nchini TFF Alfred Lucas Mapunda, amesema mchezo huo muhimu kwa Tanzania utapigwa katika uwanja huo, Julai 15 ukiwa ni mchezo muhimu kwa Taifa Stars.

Mapunda amesema kwa kuwa wanaenda kushiriki michuano ya COSAFA wamejiwekea Matumaini ya kufika hatua ya Fainali na hivyo watarejea nchini Julai 13 na kuelekea moja kwa moja mkoani Mwanza Kwa ajili ya Mchezo huo.

Ikitokea Tanzania imefanya vizuri katika michuano ya COSAFA inamaanisha kwamba tutakuwepo Afrika Kusini hadi Julai 12, hivyo Mwalimu Mayanga ameona kuwa timu ikiwa kule imalize kabisa programu za kambi kwa ajili ya mchezo na Rwanda” Alfred Lucas Mapunda Alisema.

Ikumbukwe kwamba Iwapo Tanzania itafanikiwa kuwatoa Rwanda Itakutana na Mshindi kati ya Uganda na Sudan Kusini Agosti 11 Mwaka huu.

Mashindano hayo yalianzishwa Mwaka 2009 ambapo kwa Mara ya kwanza  timu 8 kutoka Kanda Saba za Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’ zilishiriki, Huku Tanzania akifanikiwa kushiriki Lakini hakufanya Vizuri kwa kuishia hatua ya makundi.

Aidha mashindano yajayo yatafanyika nchini Kenya kuanzia January 11 hadi Februari 2 na timu 16 zinatarajia kushiriki mashindano hayo.

Video: Ndege ya Marekani, NATO yainyemelea ndege iliyombeba Waziri wa Urusi
Kamishna Siang’a asema wauza ‘Unga’ walijaribu kumuua wiki iliyopita