Bilionea anayeshika nafasi ya kwanza kwa utajiri duniani, Alon Musk amejitosa kuununua mtandao wa kijamii wa Twitter, akitoa pesa inayozidi bei iliyowekwa sokoni.

Musk ambaye ni mmiliki wa kampuni ya Esla anayetajwa kuwa na utajiri wa $273 bilioni, amewasilisha ombi kwenye Mamlaka za Biashara za Marekani akitaka kuinunua Twitter kwa $54.20 kwa hisa moja, bei ambayo ni zaidi ya iliyokuwa kwenye soko la hisa la New York ambayo ni $45.81 kwa hisa.

Hatua hiyo inaonesha kuwa Musk ndiye mtu binafsi ambaye hadi sasa ana nafasi kubwa ya kuununua mtandao huo unaotumiwa na zaidi ya watu milioni 200 kila siku.

Rais Samia afanya mazungumzo na makamu wa Rais wa Marekani

Hata hivyo, wamiliki wa Twitter wanaonesha kutomkubali Musk kuwa mnunuzi wa Twitter na wameanza kumuwekea vikwazo. Lakini bei yake aliyoiwasilisha kwenye Tume ya Marekani ya Biashara (U.S. Securities and Exchange Commission) inaonesha kuvivuka vikwazo hivyo kwa hatua ya kwanza ya tathmini.

Katika mahojiano aliyofanya Alhamisi wiki hii, Musk alisema hana uhakika kama atafanikisha nia yake ya kuinunua Twitter kutokana na kikwazo cha Bodi ya mtandao huo wa kijamii.

Musk alieleza kuwa kama hatafanikiwa kwa njia hiyo ana njia nyingine mbadala atakayotumia kufanikisha. Bilionea huyo alikataa kuielezea njia mbadala anayoifikiria.

Mwanzilishi wa Twitter, Jack Dorsey amesema kuwa hajalazimishwa kuondoka kwenye umiliki wa kampuni hiyo, aliamua kwa hiari.

Video: Kipanya aonesha mchoro wa gari lake kwa mara ya kwanza, "yajayo ni moto"
Muaddi afunguka ya Rihanna na Baba mtoto wake