Kampuni ya TECNO kwa kushirikiana Kampuni ua Tigo wamezindua huduma ya TECNO CAMON X ikiwa ni muendelezo wa toleo la ‘CAMON’ iliyoboreshwa zaidi katika upande wa kamera ikiwa na megapixel 20 na mfumo mpya wa ku-unlock simu ‘FACE ID’itakayopatikana katika maduka yote ya tigo ikiwa imeambatanishwa na kifurushi cha GB 3 kutoka mtandao wa tigo.

TECNO na Tigo kwa pamoja wameamua kuhakikisha kuwa watumiaji wa TECNO CAMON X wanafurahia huduma iliyoboreshwa.

Aidha, Kampuni ya TECNO imekua ikishirikiana zaidi na kampuni za mawasiliano kila inapokuwa na toleo jipya la simu na sasa kuendeleza utamaduni huo kupitia TECNO CAMON X,ambayo ni kubwa zaidi kulinganisha na toleo lolote la CAMON.

Akizungumza na vyombo vya habari wakati wa uzinduzi, Msemaji wa Kampuni ya TECNO, Eric Mkomoye amesema kuwa wanayofuraha kuwapelekea wateja wao huduma zenye ubora.

Hata hivyo, kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Mauzo wa Kampuni ya Tigo, David Umoh amesema kuwa dhumuni la kampuni hiyo ni kuhakikisha soko la simu linakua zaidi Tanzania.

 

Wenger afunguka kilichomsukuma kung'atuka Emirates Stadium
Chadema yapeleka ombi polisi