Magwiji wa soka la bongo, Simba SC na Young Africans SC watakutana Agosti 23, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa Ngao ya Jamii kuashiria ufunguzi wa Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara msimu wa 2017/18.

Ukweli wa mchezo huo umefahamika hii leo wakati afisa habari wa TFF , Alfred Lucas amelipozungumza na Waandishi wa Habari mjini Dar es Salaam na kuweka hadharani ratiba ya ligi kuu ambayo itaanza Agosti 26, mwaka huu.

Mabingwa wa Ligi Kuu, Young Africans watakutana na washindi wa Kombe la TFF, maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) Agosti 23 katika mchezo wa Jamii na wiki moja baadaye kitimutimu cha Ligi Kuu kitaanza.

Mechi za Ufunguzi Agosti 26 zitazikutanisha Ndanda na Azam FC Uwanja wa Nangwanea Sijaona, Mtwara, Simba SC na Ruvu Shooting Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Mwadui FC na Singida United Uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga, Mtibwa Sugar na Stand United Uwanja wa Manungu,Turiani, Morogoro, Kagera Sugar na Mbao FC Uwanja wa Kaitaba Bukoba, Nombe Mji na Tanzania Prisons na Mbeya City dhidi ya Majimaji Uwanja wa Sokoine, Mbeya.

Mabingwa watetezi, Young Africans wataanza kutetea taji lao Jumapili ya Jumapili Agosti 27 kwa kumenyana na Lipuli ya Iringa Uwanja wa Taifa, wakati Oktoba 14 watamenyana na mahasimu wao, Simba.

Mbunge wa Dokololo nchini Uganda aifagilia JKCI
Dkt. Mpango awatuliza wamachinga, awaahidi makubwa