Sababu za kuachwa kwa mshambuliaji kutoka nchini Gabon Pierre-Emerick Aubameyang katika kikosi cha Borussia Dortmund, kilichopambana usiku wa kumakia hii leo kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Sporting Lisbon zimefahamika.

Meneja wa Dortmund Thomas Tuchel alibanwa na waandishi wa habari mara baada ya mchezo huo, ambao ulimalizika kwa Sporting Lisbon kufungwa bao moja kwa sifuri, na kuulizwa kwa nini hakumtumia mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27.

Tuchel alisema hakumchezesha Aubameyang, kutokana na sababu za ndani, hivyo hakutaka kuingilia uhuru wa mtu.

Tuchel alisema “Suala kubwa hapa ni kuheshimu maamuzi ya muhusika, lakini ninawahakikishieni Aubameyang atakuwa sehemu ya kikosi changu katika mchezo wa ligi ya Bundesliga dhidi ya Hamburg mwishoni mwa juma hili.

Nafasi ya mshambuliaji huyo katika mchezo wa usiku wa kumkia hii leo ambao uliunguruma mjini Dortmund, ilichukuliwa na Adrian Ramos ambaye aliifungia bao pakee na la ushindi.

Aliyemchinja mkewe na kutoweka ajisalimisha apate ARV
Jose Mourinho Ahukumiwa, Kukaa Jukwaani Liberty Stadium