Timu ya soka ya TPB Bank FC imefanikiwa kuikung’uta timu ya waandishi wa habari za michezo nchini, Taswa FC baada ya kuifunga kwa mabao 3-2.

Mchezo huo maalum, ulifanyika kwenye uwanja wa Shule ya Sheria (Law School) uliopo maeneo ya kituo cha mabasi cha Mawasiliano jijini Dar es salaam na timu zote mbili zilishambuliana kwa zamu.

TPB Bank FC ilitumia  idadi pungufu ya wachezaji wa Taswa FC kufunga mabao yote katika mchezo huo ambao pia ulikuwa wa maandalizi kwa timu hiyo ya benki kuelekea katika mashindano ya soka ya taasisi za kibenki yanayotarajiwa kuanza hivi karibuni.

Aidha, bao la kwanza la TPB Bank FC lilifungwa na nahodha wa timu hiyo, Baraka Kyomo  katika dakika ya 10 ya mchezo  baada ya kuwashinda kasi mabeki wa Taswa FC na kufunga kirahisi.

Hata hivyo, Taswa FC ilianza harakati za kusawazisha mabao hayo kuanzia kipindi cha pili baada ya kutimia wachezaji wote 11. bao la kwanza la Taswa FC lilifungwa na Fred Pastory baada ya kupokea pasi safi ya Zahoro Mlanzi kabla ya Shedrack Kilasi kufunga la pili kufutia mpira wa kona wa Juma Ramadhani.

 

Video: Mpina awapa miezi mitatu DAWASCO kurekebisha miundo mbinu yao
Magazeti ya Tanzania leo Julai 9, 2017