Rais wa Marekani, Donald Trump amesema kuwa kwasasa ni vyema walimu wakapatiwa silaha ili kuweza kukabiliana na mashambulio ambayo yamekuwa yakitokea mara kwa mara mashuleni.

Ameyasema hayo alipokuwa katika mjadala maalumu uliofanyika Ikulu ya Marekani, ambapo uliwashirikisha wanafunzi na wazazi walioathirika katika mashambulizi ya bunduki nchini humo.

Aidha, Mjadala mkali umeibuka juu ya umiliki wa silaha nchini humo kufuatia shambulizi la bunduki lililofanywa na Nikolas Cruz wiki iliyopita katika shule ya sekondari ya Marjory Stoneman Douglas na kuuwa watu 17 katika jimbo la Florida.

“Mwalimu mwenye bunduki anaweza kukabiliana na washambuliaji mara moja, anaweza kusitisha shambulizi lolote kwa haraka. lakini napendekeza wapewe mafunzo maalum ili waweze kusaidia hili,”amesema Trump

Hata hivyo, Majimbo kadhaa nchini Marekani tayari yanaruhusu mtu kumiliki bunduki ndani ya vyuo na taasisi za elimu.

Raia wazidi kutaabika nchini Burundi
Video: Saa 120 za patashika msiba wa Akwilina, Chadema yazidi kubomoka