Wengi wetu hutafsiri zawadi kwa namna tofauti, iaminike kuwa zawadi si kuhonga au kujipendekeza kwa mpenzi wako akupende zaidi, zawadi kwa mpenzi wako ni mvuto wa hiari utokao moyoni kwa lengo zuri juu ya mwenza wako, tafsiri nne ya kumpa zawadi mpenzi wako.

1.Huimarisha uhusiano na kuongezeka mapenzi ya kweli.
Pindi utoapo zawadi kwa mwenzi wako, mwenza huyo hujihisi yeye ni wa thamani sana mbele yako.  kwani zawadi hutafsiriwa na mpokeaji kama ni mtu wa thamani sana,   mtu ambaye anapendwa kweli hivyo pindi ufanyapo kitendo cha utoaji wa zawadi yeyote ile kwa mwenzi wako, hufanya mahusiano yenu yaimarike na si kuteteleka.

2. Humfanya mtu ajihisi yupo mahali salama.
zawadi hutafsiwa na mpokeaji ya kwamba yupo mahali sahihi, kwani kitendo cha mtu kukufikiria bila shinikzo la mtu yeyote ni jambo jema kwani hufanya ujisikie ni mtu unayehitaji faraja na uthamini, Hivyo ili kuweza kuudumisha upendo wako na mwenzi wako jenga utaratibu wa kumpa zawadi mpenzi wako

3. Zawadi huacha kumbukumbu.
Hakuna kitu ambacho huacha alama kubwa katika mahusiano kama zawadi. Hivi hajawahi kukutana na mtu anamwambia ya kwamba kitu hiki alinipa fulani?  Bila shaka umewahi kukutana na mtu wa aina hiyo.  Kama ndivyo hivyo amini ya kwamba zawadi huacha alama katika mahusiano.

4. Huonesha upendo wa hali ya juu.

Ni kweli kwani kitendo hiko hudhirisha wazi kuwa mpenzi wako hukutakia tabasamu, amani kila umuonapo.

Ifahamike kuwa kitendo cha kutoa zawadi katika mahusiano ni jukumu la wote wawili mume a mke, wengi hufikiri mwanaume pekee ndio jukumu lake la hasha, wanawake wajifune kuridhika na kile ambacho mwanaume amejipinda kukifanya kwa lengo la kumfurahisha haijalishi kiwe kikubwa namna gani au kidogo ni namna gani.

Mwinjuma muhumini amewahi kuimbaa akisema, zawadi ni zawadi chukua iwe mbaya au nzuri zawadi ni zawadi iwe kubwa au ndogo zawadi ni zawadi.

Sakata la Korosho kaa la moto bungeni, 'Mbunge aahidi kujiuzulu'
Neema Mgaya akerwa na mauaji Njombe,'Huu ukatili hauvumiliki'

Comments

comments