Tangazo alilolitoa kiongozi wa chama cha ANC Musalia Mudavadi katika mkutano wa wajumbe wa chama hicho siku ya Jumapili tarehe 23 Januari 2021 lingesababisha tetemeko la ardhi la kisiasa ambalo lingepanga upya na kurekebisha hali ya kisiasa ya nchi ya Kenya inapojiandaa kuelekea uchaguzi Mkuu wa Agosti 2022.

Kiongozi wa chama cha ANC nchini Kenya, ni miongini mwa viongizi wakuu wa Muungano wa One Kenya Alliance (OKA), ambao ni muungano wa waliokuwa wanachama wakuu wa National Super Alliance (NASA), jukwaa la kampeni ambalo lilitumika katika uchaguzi wa 2017

Viongozi hao ni pamoja na aliyekuwa Makamu wa Rais Mhe. Kalonzo Musyoka -kiongozi wa chama cha Wiper, Mhe. Seneta Moses Wetangula, kiongozi wa Ford-Kenya na Mheshimiwa Seneta Gideon Moi, kiongozi wa KANU.

Kuundwa kwa OKA kulitokana na kutoaminiana na dhuluma ambazo viongozi hawa waliamini zilisababishwa na aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga na mshirika wao wa NASA.

Uongozi wa OKA uliamini kuwa wangeweza kuweka waziwazi njia mbadala ya kisiasa, mbali na siasa zinazodhaniwa kuwa sumu ambazo zilikuwa zikiwazunguka Raila Odinga na Naibu Rais William Ruto.

Kama sehemu ya kujenga moyo wa urafiki na mshikamano miongoni mwa vyama vinavyounda OKA, viongozi wa chama hicho walikubali kuhudhuria na kushuhudia kila mkutano mkuu wa wajumbe wa vyama hivyo (NDC).

Mkutano wa NDC umekuwa chombo cha juu zaidi cha kufanya maamuzi katika chama chochote cha siasa ambacho kingewapa viongozi wa chama mamlaka mapya ya kutafuta washirika wapya wa kisiasa katika harakati za kupata urais/mamlaka ya kisiasa. Kwa hivyo walihudhuria mikutano ya NDC ya kila mmoja wao kama walivyokubaliana.

Hivyobasi kwa upande wa ANC, kama ilivyokuwa katika vyama vingine, wakuu wa muungano wa OKA walialikwa na kama kawaida walihudhuria

Hatahivyo ni wakati wa mkutano huo wa NDC Uhudhuriaji wa wanachama wengi wa chama cha UDA na maseneta uliofuatiwa na ujio wa naibu wa Rais William Ruto ambaye ndiye kiongozi wa UDA , uliwashangaza wengi, waliokuwa katika ukumbi wa Bomas na hata wale waliokuwa wakitazama kupitia vyombo tofauti vya Habari.

Mudavadi kutokana na kuwaalika Naibu Rais William Ruto na waandamizi wake wa UDA aliwaonyesha wanasiasa kwamba hakuna kitu cha kudumu isipokuwa maslahi katika siasa.

Uchaguzi Mkuu wa kitaifa bila shaka utakuwa wa mbio za farasi wawili kati ya mrengo wa kisiasa unaomuunga mkono Raila Odinga (Azimio) na mrengo mpya wa kisiasa unaoongozwa na Naibu Rais William Ruto akiungwa mkono na Musalia Mudavadi na Moses Wetangula.

Wakuu wawili waliosalia OKA kwa hivyo watalazimika kuchagua upande gani wa mgawanyiko wa kisiasa kuunga mkono.

Kuondoka kwa vigogo hao wawili kutoka Muungano wa NASA na taarifa yao waliotoa katika mkutano huo wa wajumbe wa chama cha ANC kwamba watatafuta washirika wapya kuelekea uchaguzi mkuu wa 2022, na sio muungano wa Azimio, lilikuwa tetemeko la tatu la siku.

Kufuatia taarifa hiyo, lile ambalo lilionekana kuwa ngome ya Raila, ilibadilika na kuwa eneo ambalo naibu wa rais Wiiliam Ruto atapigania kuliweka katika kikapu chake kupitia usaidizi wa Musalia Mudavadi Moses Wetangula.

Young Africans yatua Mwanza kuikabili Mbao FC
Uchaguzi Kenya2022:Kenyatta amtaka Raila kuwa mrithi wake