Shirikisho la soka barani Ulaya ‘UEFA’ limemfungia kucheza michezo mitatu mlinda mlango Gianluigi Buffon baada ya kumshambulia kwa maneno mwamuzi Michael Oliver aliyechezesha mchezo wa klabu bingwa barani Ulaya baina ya Juventus na Real Madrid ambapo Juventus aliondolewa katika nusu fainali.

Buffon aliondolewa katika mchezo huo kwa kadi nyekundu baada ya kumtolea maneno makali mwamuzi kufuatia mwamuzi kutoa penati kwa Madrid sekunde chache kabla ya mchezo huo kumalizika.

Baada ya mchezo huo kumalizika Buffon alieza kutofurahishwa na maamuzi ya refa huyo akienda mbali na kusema mwamuzi Michael Oliver hana moyo isipokuwa ana mzigo wa uchafu.

Katika mchezo wa awali Madrid walishinda mabao 3-1 dhidi ya Juventus na katika mchezo wa pili wakati mwamuzi anaizawadia penati Real Madrid tayari Juventus walikuwa mbele kwa mabo 2-0 hivyo penati iliyopigwa na Ronaldo na kutinga wavuvuni ilifanya matokeo kuwa 4-3, matokeo yaliyoifanya Madrid kutinga fainali.

Tayari Gianluigi Buffon alishitangaza kuondoka Juventus baada ya kuitumikia kwa miaka 17 lakini mlinda mlango huyo hatatundika daruga.

 

 

 

 

 

Magazeti ya Tanzania leo Juni 6, 2018
Wabunge wazibwa midomo kuhusu Trilioni 1.5